Friday, July 18, 2014

LULU ATIA TIMU UKUMBINI KUISAKA NAMBA YA SIMU YA JUSTIN BIEBER....SHUKA NAYO

Vile vituko vya reja reja kutoka kwa Tanzanian star actress Elizabeth Michael “Lulu” bado vinaendelea.
 
Habari mpya zinasema kuwa juzi Lulu alienda kwenye seminar ya kuzungumza na wasanii wa Tanzania namna ya kukuza sanaa ya nchini huku watoa mada wakubwa wakiwa mastaa wa Marekani Terrence J, David Banner na Shaka Zulu…
justine bieber
 
Kwa mujibu wa vyanzo  vyetu, lengo kubwa la Lulu kuhudhuria seminar hiyo ilikuwa kupata namba za Justine Bieber ambaye amekuwa akiukosha moyo wake kwa miaka takribani 3 sasa. 
Elizabeth Michael ‘Lulu’
Elizabeth Michael ‘Lulu’

Katika semina hiyo inadaiwa kuwa baada ya jina la Bieber kutajwa, Lulu alishtuka na kuushikilia moyo wake kuonyesha ni ni jinsi gani amemuingia moyoni kama si rohoni huku Bieber mwenyewe akiwa hata hamjui Lulu.
 
Hata hivyo Lulu alipoulizwa na gazeti moja alidai kuwa hakumaanisha moja kwa moja kutaka namba za Bieber licha ya kumzimikia na siku za nyuma kudai yupo tayari kwa lolote akikutana na Bieber