Monday, July 21, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI KIONGOZI MPYA WA MAHAKAMA KUU





 
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:
 
 255-22-2114512, 2116898
 
 E-mail: ikulucommpress@googlemail.co Website : www.ikulu.go.tz  Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
 
STATE HOUSE,1 BARACK OBAMA ROAD,11400 DAR ES SALAAM.Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. JakayaMrisho Kikwete, amemteua Mheshimiwa Jaji Shabani Ally LILA (53) kuwa JajiKiongozi wa Mahakama Kuu kuanzia tarehe 21 Julai, 2014. Jaji Kiongozi Mteule, Mhe. Jaji Shabani Ally LILA, anajaza nafasiiliyoachwa wazi na Mheshimiwa Jaji Fakih A.R. Jundu ambaye anastaafu kwamujibu wa Sheria
leo tarehe 20 Julai, 2014.
 Jaji Kiongozi Mteule ana uzoefu wa miaka ishirini na miwili (22) katikaMahakama ya Tanzania. Amefanya kazi kwenye Mahakama kama ifuatavyo:-1992
 1995 Hakimu Mkazi, Tanga1995
 1998 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lindi1998
 2000 Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, KandaYa Songea.2000
 2002 Hakimu Mkazi, Mkoa wa Lindi2002
 2003 Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, KandaYa Mbeya.2003
 2005 Hakimu Mkazi na Msajili wa Mahakama Kuu, KandaYa Dar es Salaam.2005
 2006 Hakimu Mkazi, na Msajili wa Mahakama Kuu, KandaYa Arusha.
 
2006
 2008 Jaji wa Mahakama Kuu,Kanda ya Dodoma2008
 2013 Jaji wa Mahakama Kuu, na Jaji Mfawidhi, Kanda yaMtwara2013
 2014 -Jaji wa Mahakama Kuu, Masijala Kuu, akishughulikiauanzishwaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Ilala.Mheshimiwa Jaji Shabani Ally LILA ana Shahada ya Sheria (LLB Hons) yaChuo Kikuu cha Dar es Salaam alikohitimu mwaka 1991 na tangu wakati huoamehudhuria kozi fupi, mikutano, semina na makongamano mengi kwenyeeneo lake la kazi. Ni mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Majaji na Mwenyekiti waKamati ya Taifa ya Huduma za Jamii (Wafungwa).Katika kumteua Mhe. Jaji Shabani Ally LILA kuwa Jaji Kiongozi waMahakama Kuu, Rais ameridhika kuwa ni mweledi, mchapa kazi, mzalendo,muadilifu na kwamba atakuwa msimamizi na kiongozi imara wa MahakamaKuu na Mahakama za chini na anamtakia kazi njema.Aidha, Mheshimiwa Rais, anamshukuru sana Mheshimiwa Jaji KiongoziMstaafu, Mhe. Fakih A.R. JUNDU kwa utumishi wake mzuri na mrefu katikaMahakama kwa ujumla na kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano alichokuwa Jaji Kiongozi na anamtakia kila la kheri katika shughuli zake nyingine.Mwisho!
Balozi
 Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI
Imetolewa na;Premi Kibanga,Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
IKULU - DAR ES SALAAM.
20 Julai, 2014