Friday, July 25, 2014

SHEHE AWAVAA WEMA, DIDA!, NI KUHUSU KUWEKA KAUNTA ZA POMBE NYUMBANI

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum (pichani kushoto), amewavaa baadhi ya mastaa Waislamu wa Kibongo wenye kaunta zenye pombe majumbani mwao hasa kwa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku akiwataka waondoe mara moja kwani ujana unawasumbua, Ijumaa lina ripoti kamili. 
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum
WAMO DIDA, WEMA & DIAMOND
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya mastaa Waislamu wenye kaunta zenye pombe majumbani mwao kuwa ni pamoja na Mtangazaji wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Akizungumza na Ijumaa mapema wiki hii jijini Dar es Salaam, Shehe Salum alisema kwamba, kwanza ameshtushwa na habari ya hao wanaojiita mastaa kuwa na kaunta za pombe majumbani kwao kwani ni habari ngeni masikioni mwake na kusema kuwa kwa semina wanayoipata mwezi huu hawatakiwi kutenda maovu.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
WANAPASWA KUOMBA DUA
Alisema kuwa mastaa hao wanapaswa kuutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kusoma Quran, kuomba dua na kuacha maovu yote.
“Hao mastaa wenye kaunta wanatakiwa kuacha na kuondoa kabisa kwani Ramadhani imeletwa kwetu kama semina na hatutakiwi ikiisha turejee kule tulipokuwa.
“Mafunzo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani maana yake tujifunze na tuachane na kule tulikotoka, hivi kwa nini wasijiulize mastaa wenzao wako wapi kwa mfano Sharo (mchekeshaji Sharomilionea) na wengine waliotangulia mbele ya haki?
WANAKULA UJANA?
“Wasijidanganye na ujana walio nao, wakikutwa na mauti, mbele ya haki watasema nini?
“Nawaasa kutorudi nyuma na kujifunza kwelikweli namna ya kuishika dini na nguzo zake,” alisema shehe huyo.
Baa ya ndani ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
SWAUMU ZAO VIPI?
Shehe mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake anayeswalisha katika msikiti uliopo Sinza jijini Dar alisema:
“Kiukweli kabisa pombe ni haramu na hatutakiwi  kuikaribia hata kidogo. Hawa ambao wamefikia hatua ya kuwa na kaunta za pombe majumbani kwao, wanakosea sana.
“Kwa mfano mwezi huu mtukufu kama wanafunga, si kwamba hawapati thawabu, wanapata ila kwenye kuikaribia pombe, watakuwa wanapata dhambi.
“Kwa hiyo unaweza kuwa umefunga lakini ukashangaa mpaka mwezi umeisha thawabu zako zimepungua kutokana na mambo mengine yanayokufanya upate dhambi.”
Mtangazaji wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’,
DIDA ANASEMAJE?
Baada ya Shehe Salum kuwavaa mastaa hao, gazeti hili lilimsaka mmoja baada ya mwingine.
Alipopatikana, Dida ambaye ni binti wa Kiislamu mwenye kaunta ya pombe nyumbani kwake, Mwananyama, Dar alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli mimi nina kaunta ndani kwangu lakini kwa mwezi huu hata mimi naichukia sana pombe na sipendi kabisa kuiona pamoja na kwamba sijui sana sheria za dini japo ni muhimu kuzijua nguzo zake.
“Hata mimi kama binti wa Kiislamu kwa mwezi huu mtukufu sinywi pombe na hiyo kaunta ni kwa ajili ya wageni wangu wanaonitembelea.”
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
NYUMBANI KWA DIAMOND
Wiki mbili zilizopita ishu hiyo ilitibua futari nyumbani kwa Diamond maeneo ya Sinza-Mori, Dar hivyo kulazimika kuondoa pombe kali zilizokuwa zimejazwa kwenye kaunta.
WEMA VIPI?
Kwa upande wake Wema ambaye ukiingia kwake kitu cha kwanza unakutana na kaunta ya pombe na vinywaji vingine alipotafutwa ili kuzungumzia ishu hiyo, simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.