Thursday, August 14, 2014

TAARIFA KUTOKA KWA AFANDE SERE JUU YA KIFO CHA MAMA WATOTO WAKE


Selemani Mshindi maarufu kwa jina la Afande Sele amewajulisha watu wake wa karibu na mashabiki kuhusu msiba uliomkuta kwa kufiwa na mama wa mwanae Tunda.

 Kupitia ukurasa wa facebook Afande Sele aliandika “Ndugu zangu!! Nimefiwa na mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. Sisi ni waja wa mwenyezi mungu na hakika kwake tutarejea; mungu ampumzishe pema.”
AFANDE