Saturday, September 20, 2014

BAADA YA KUPATA LAANA YA MAREHEMU KANUMBA,CATHY ADAI BONGO MUVI INAKUFA

Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Msanii wa filamu Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.
“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.