Thursday, October 2, 2014

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA:LINEX AVULIWA NGUO ZA KIJESHI ALZO ZIVAA NA WANAJESHI LIVE

Kitu kama hiki kiliwahi kumtokea mwanahiphop Young Killer miezi michache iliyopita ambapo alivuliwa nguo ya jeshi aliyokua ameivaa…. wiki kadhaa baadae ikatangazwa tena kwenye vyombo vya habari kwamba ni marufuku kwa watu wasio Wanajeshi kuvaa nguo hizo.
Mwingine aliekutwa na mkasa huu ni msanii Linex akiwa Mbeya ambapo imefahamika  Wanajeshi walilazimika kuichukua suruali ya jeshi tukio lililomfanya ahojiwe na Soudy Brown leo na kujibu >>>‘nilikua nimevaa kama zinataka kufanana na nguo za jeshi, zinataka kufanana kwa mbali lakini sio nguo ya jeshi‘
Kwenye sentensi nyingine Linex akasema >>> ‘sikutaka kuwa mtata jamaa walikuja wakasema ile ni nguo yao nikaingia kwenye gari iliyokua imenipeleka Airport pale nikavua nikawapa sababu lazima niliheshimu jeshi la nchi yangu‘
Linex

‘Big up kwa Wanajeshi waliofanya vile labda mimi ndio nilitakiwa kuwa mfano kwa watu wengine wanaozivaa mtaani, kwa ushauri tu ni kwamba Wanajeshi wapite kwenye maduka pia yanayouza nguo zinazofanana na nguo zao wachukue’ – Linex