Thursday, March 26, 2015

IRENE UWOYA ALIA NA WASICHANA WANAOTOA MIMBA

Irene Uwoya
Staa mrembo kutoka Bongo Movies,amewaasa wanawake  kuacha kutoa mimba hata kama  watakumbana na mtatizo,kwani mtoto ndio kila kitu katika maisha.

Msanii huyu alitoa wito huo hivi juzi kati akiwataka  wajawazito wote waliokataliwa  na wapenzi wao kuonyesha kuwa  wao  ni wanawake majasiri  kwa kutothubutu kutoa mimba hizo.

Mtoto  ni zawadi  kutoka kwa  Mungu, siku ya leo  nawashauri wanawake  wanaokataliwa  mimba na wapenzi wao wasitoe wala kufanya  chochote muonyeshe kama wewe ni mwanamke jasiri na unaweza, mtoto ndio kila kitu, ‘plzzzz’ usitoe mimbaaa’. Alisema.

Kufuatia ujumbe huo baadhi ya mashabiki wake  walionekana  kumuunga mkono  mrembo huyu ambae ni mama wa mtoto mmoja.