Sunday, May 31, 2015

CHEKA NOMA! AMPIGA MTHAILAND KWA TKO, AMTOA VIDAMU PUANI

Singwacha akiandaliwa na msaidizi wake dakika chache kabla ya pambano kuanza.
Cheka akimtifua Mthailand.
Pambano likiendelea.
Sehemu ya mashuhuda wachache waliohudhuria pambano hilo.
Vidamu vikimchirizika Mthailand wa watu baada ya kuchezea ‘kabasero’.
BONDIA Francis Cheka jana aliendeleza ubabe kwa kumchapa bondia Kiatchai Singwancha kutoka Thailand katika pambano lililofanyika Ukumbi wa PTA uliopo Viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Pambano hilo Cheka alilimaliza katika raundi ya nane baada ya kumteua bega mpinzani wake.