Saturday, June 13, 2015

Picha za Aliyekuwa Mke wa Bob Junior Akiwa na Mpenzi wake Mpya Nimekuwekea Hapa

 Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka studio ya Sharobaro Records,Bob Junior ambaye alimpa talaka mkewe,aitwaye Halima Ally miaka kadhaa iliyopita baada ya kushindana tabia,hatimaye ‘mkewe’ amepata mpenzi mpya aitwaye Immu Bella.

Picha kadhaa ambazo Clouds.com imezipata zikimuonyesha Immu Bella ambaye ni msanii wa Bongo Fleva akiwa na aliyekuwa mke wa Bob Junio huku amembeba mtoto wa msanii huyo.

Mwanaume huyo akizungumza na Clouds Fm,alisema kuwa ni kweli Halima ni mpenzi wake na wana mipango endelevu ya penzi lao na yuko tayari kumlea mtoto wa Bob Junior kwa kuwa hana hatia yoyote.