Monday, August 31, 2015

Kwa Hili Alilolifanya Diamond, Litamgharimu Sana Katika Safari Yake ya Kimuziki

Diamond platnumz kaonesha wazi
msimamo wake katika mgonbea
anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi
yake, ila naona kama alikurupuka kufanya
maamuzi hayo. Diamond angetambua kuwa
washabiki wake wengi wanaompa support
hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye.
Nimepitia baadhi ya comments za followers
wake na kugundua kuwa 90% wamekuwa
disappointed sana na alichokionesha.
Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi
baada ya ile hafla yao na mheshimiwa.
Maana baada ya pale wasanii kibao
wamekurupuka kuonesha support kwa
Magufuli.
Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki
wameanzisha kampeni ya kutomsapport
tena Diamond kwa kuacha kumpigia kura
katika tunzo anazoshindania.