Monday, August 31, 2015

Masogange: Siishi kwa makalio yangu


Video Queen wa Kibongo, Agness Gerald ‘Masogange’ amewabwatukia watu wanaomsonga na maneno kuwa anaishi mjini kwa kuyanadi makalio yake mtandaoni.

Akizungumzia  madai  hayo, Masogange amesema kuwa umbo lake amejaliwa na Mungu na halitumii kama vile wengi wanavyodhani kuwa anajinadi kwenye mitandao ili kuwakamata midume.
  
“Watu wengine sijui wakoje, kila mtu ana mfumo wa maisha yake anavyotaka kuishi, siyo kwamba naishi mjini kwa sababu ya makalio yangu, wanaodhani hivyo wanakosea sana,” alisema Masogange.