KABAANG! Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amenaswa kimalovee na rafiki wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku ikidaiwa ni ‘mtu’ wake.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba jamaa huyo ambaye anajiita Dangote Kifyagio ni rafiki wa Diamond ambaye alikuwa akimsaidia mambo yake kimuziki ili awe juu.
“Unajua yule Kifyagio alikuwa rafiki wa Diomond sana huko nyuma, sasa isije ikawa kaamua kujiweka kwa shemeji yake maana si unawajua tena hawa mastaa wetu, nyie fuatilieni mtaujua ukweli.”
“Halafu sikia nikwambie, vitu vingine ni upuuzi tu hivyo vitu vinaniharibia deal zangu na mipango yangu yote, sipendi hata kidogo, yaani sipendi kwanza kufuatiliwa, amekuwa mtu wangu? Nishawahi kumposti na kusema ni bwana’angu zaidi ya mimi na yeye kuheshimiana? Nina bwana wangu ambaye ndiye kila kitu kwangu jamani sipendi wallah…sipendi.”