Wednesday, September 2, 2015

MHE.JANUARY MAKAMBA ASHANGAZWA NA HAYA MAGAZETI MATATU KUHUSU LOWASSA

makamba

Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameonesha kushangazwa na mfanano wa vichwa vya habari vya magazeti ya leo kuhusu mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Makamba ambaye ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, ameonyesha kurasa za mbele za magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Tanzania Daima zilizokuwa na vichwa vya habari vinavyomnukuu Lowassa akitaka watanzania wasiogope.
Amepost picha za magazeti hayo kwenye twitter na kuhoji kama mfanano huo ni bahati mbaya au imeratibiwa?