Wednesday, September 30, 2015

TAZAMA VIDEO ZA MAGOLI LIGI YA MABINGWA ULAYA ILIYOPIGWA HAPO JANA

September 29 michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, miongoni mwa mechi zilizovuta hisia za watu wengi ni mechi ya Arsenal dhidi ya Olympiakos, mechi ambayo ilimalizika kwa klabu yaArsenal kupoteza mechi hiyo katika uwanja wake wa nyumbani kwa jumla ya goli  2-3.
Video ya magoli ya Arsenal 2-3 Olympiakos
Mchezo mwingine uliokuwa ukivutia ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Bayer Leverkusen mechi ambayo ilimalizika kwa klabu ya FC Barcelona kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-1 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Camp Nou.
Video ya magoli ya FC Barcelona 2-1 Bayer Leverkusen
FC Bayern Munich walikuwa wenyeji wa Dinamo Zagreb katika uwanja wa Allianz Arena, mchezo ambao ulimalizika kwa FC Bayern Munich kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli kwani ilishinda jumla ya goli 5-0.
Video ya magoli FC Bayern Munich 5-0 Dinamo Zagreb
Klabu ya Chelsea chini ya kocha wake Jose Mourinho walisafiri hadi Ureno kuifuata FC Porto katika uwanja wa Estadio do Dragao, mahali ambapo Jose Mourinho ana historia na heshima kubwa katika uwanja huo ila kwa bahati mbaya Chelsea walipoteza mchezo huo kwa jumla ya goli 2-1.
Video ya magoli FC Porto 2-1 Chelsea
U