Stori za wasanii kushiriki kwenye kutengeneza video za utupu zimekuwa zikiongezeka mara kwa mara… mwaka 2007 tuliipata ya Kim Kardashian na msanii wa R&B Ray J, badaae tukaipata ya mwanamieleka Hulk Hogan na nyingine zikafuata… na pengine time hii video ya namna hiyo inayomhusu Lil Wayne ipo njiani!
Kuna stori inasambaa kwenye mitandao wakati huu kuhusu video ya utupu ya Lil Wayne, mtu asiyejulikana jina amekuwa akijaribu kuuza video hiyo ya Lil Wayne kwenye kampuni ambazo zinajihusisha na biashara za kuuza na kununua picha na video za utupu!
Website ya TMZ ya Marekani imeandika: >>> “Tunaambiwa kuwa kampuni hizi kubwa zimetafutwa na mtu mwenye hiyo video ambayo inamuonyesha Lil Wayne akiwa mtupu na soksi za miguuni tu huku wanawake wawili kwenye video hiyo wakifanya kila kitu… msemaji wa Lil Wayne amesema kama kuna video hiyo ya rapper huyo basi msanii huyo hakujua kama anarekodiwa, na wameahidi kwenda na mtu huyo sawa na Sheria ikiwa video hiyo itawafikia umma!”. <<< TMZ.
Hata kama ikitokea kampuni yoyote kununua video hiyo, hawatoweza kufanya biashara wala kuisambaza video hiyo kwa umma bila ridha ya Lil Wayne mwenyewe, kesi ambayo ipo tofauti kidogo na kesi ile ya Kim Kadarshian ya mwaka 2007 ambapo yeye alidai kuwa video yake ya utupu na msanii wa R&B Ray J ilivujishwa, kitendo ambacho kwa kipindi hicho kilimpatia Kim Kadarshian fidia zaidi ya dola milion 5 kitu kama Bilion 10 za Tanzania kwa sasa!