Friday, February 12, 2016

Linah Na Madai Ya Kumshobokea Wizkid

lina1
Mwanamuziki Linah.

Hivi karibuni kulikuwa na habari ya Mwanamuziki Linah kudai kuwa, wakati akiomba kufanya kazi na msanii kutoka Nigeria, Wizkid, mshkaji huyo aliomba atumiwe picha sexy kwanza, jambo lililoashiria kuwa kavutiwa na mtoto huyo mzuri.

Hata hivyo, licha ya Linah kudai jamaa ndiye aliyekuwa akiashiria kumtaka, rafiki wa karibu wa Linah amekisanua kuwa, dada yetu huyo ndiye ambaye amekuwa akishoboka kwa kumtumia meseji zinazoonesha kuwa, anam-love.
Wizkid1
“Meseji zake na Wiz nimeziona, Linah anaonekana kumpenda Wiz na ndiyo maana jamaa akaona aombe picha amuone yukoje ili asije akamkubalia demu kituko,” kilianika chanzo.