Thursday, April 7, 2016

Meya Dar Atoa Mpya Ya Mwaka Aikataa Nyumba Ya Serikali

   
Meya wa Dar es salaam kupitia tiketi ya CHADEMA Mhe.Charles Mwita 

Meya Mpya wa jiji la Dar es salaam Mhe.Charles Mwita (CHADEMA)ametoa kali ya mwaka na kuwashangaza watu baada ya kugoma kuhamia kwenye nyumba ya serikali ambayo ni maalumu kwa ajili ya Meya na kudai kuwa ataendelea kubakia kwenye makazi yake yaliyopo huko Vijibweni, Kigamboni.
Hata hivyo Meya huyo hakuweza kubainisha sababu yeyote muhimu iliyomfanya kuikataa nyumba hiyo aliyopewa na Serikali na kusisitiza aachwe abaki kwake Vijibweni.