Tuesday, June 24, 2014

PICHA 5 ZA TATOO ALIZOCHORA SHETTA NA SABABU ZAKE.

 
Msanii Shetta wa bongofleva anaemiliki mawimbi na single yake ya ‘kerewa’ ft. Diamond Platnumz….. amechora tatoo tano kwenye mwili wake kutokana na mambo yake muhimu maishani.
 Tatoo moja ameandika ‘muziki ni maisha yangu’ huku maneno yakiwa ndani ya gitaa kwa sababu za msingi kwamba kiukweli muziki ndio umemtoa yeye kwenye maisha yake hata kama kuna biashara nyingine anafanya, zimetokana na muziki.
 Shetta 4Tatoo ya pili ni kama kikaratasi ambacho ndani yake kuna maneno yanayomuhusu Mama yake mzazi ambae sasa ni marehemu ‘Rest in peace mama 1973-2006′
Tatoo ya tatu ina alama ya muziki juu ya bega, kuna nyingine kama drip alafu sindano yake ni kama waya wa mic…
 Tatoo nne zote amechora kwenye mkono mmoja wa kushoto amezichora South Africa wiki kadhaa zilizopita na moja iliyobaki aliichorea hapa Tanzania Sinza Dar es salaam ambayo ameiandika jina la mtoto wake wa kwanza na pekee aitwae Qayllah.
 Shetta 5
 Shetta 2
Shetta 1