Monday, July 21, 2014

CHADEMA, CCM WAMGOMBEA DUDE. KISA AMETANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE

VITA! Baada ya kutangaza nia ya kugombea ubunge, staa wa sinema Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amesema anapata wakati mgumu kwa kuwa vyama vikubwa vya siasa vinamgombea.
Staa wa sinema Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
 Akizungumza na mwanahabari wetu, Dude alisema kuwa awali alikuwa agombee kupitia Chadema, lakini baadaye CCM nao kupitia kiongozi mmoja mwenye wadhifa mkubwa serikalini alimtaka agombee kupitia tiketi ya chama hicho, jambo linalomfanya abaki njia panda.
“Nipo njia panda maana Chadema wamenipa jimbo la kugombea huku kwa upande mwingine CCM nao wamenitaka nigombee kupitia chama chao yaani kwa sasa sijui cha kufanya kabisa,” alisema Dude.