Monday, July 21, 2014

BASI LA AM COACH LAPINDUKA WILAYANI MASWA, SOMA HABARI KAMILI HAPA


Basi la AM Coach likiwa eneo la tukio katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu

Habari za hivi punde  zilizoufikia mtandao huu wa Malunde1 blog ni kwamba Basi la AM COACH lililokuwa linatoka Meatu mkoani Simiyu  kwenda Mwanza limepinduka katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu.


Kwa mujibu wa habari kutoka eneo la tukio watu sita wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwani hali za ni mbaya.