Monday, July 21, 2014

HABARI MBAYA: JULIANA KANYOMOZI AMPOTEZA MTOTO WAKE WA KIUME

Juliana-Kanyomozi2-post
Mwanamuziki maarufu wa nchini Uganda, Juliana Kanyomozi,jana asubuhi amempoteza mtoto wake mdogo wa kiume Keron baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Pumu. Kwa mujibu wa gazeti na New Vision Keron amefariki katika hospitali ya Aghakhan.
Kanyomozi
Ni wakati mgumu kwa mwanamuziki huyo mrembo kwakuwa amekuwa akimpenda sana mtoto wake wakati akithibitisha taarifa hizo.
New Vision imemnukuu Juliana akisema kuwa” Malaika wangu ametangulia kwa Mungu, kilichosambazwa awali ni uzushi. Amefariki jana saa 10:25 asubuhi, amekuwa mpambanaji mkubwa wa afya yake nawashukuru wote kwa maombi yenu nitajitahidi kujikaza, Mungu amlaze mahali pema Keron lala salama mwanangu hadi tutakapokutana tena.”
Juliana amewaomba mashabiki wake kumuombea mtoto wake huyo haswa katika kipindi hiki kigumu kwake.
Juliana amesema mtoto wake hakuwa katika hali nzuri baada ya kushambuliwa na ugonjwa wa Pumu uliomsababishia kupoteza maisha.