Monday, July 21, 2014

NISHA: NIACHENI NA MAMA YANGU YEYE NDO SHOSTI WANGU MKUBWA KWASASA WENGINE WOTE WANAFIKI!!

Vunja ukimya! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amevunja ukimya kwa kusema kuwa kwa sasa hana shosti zaidi ya mama yake mzazi.
Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Akifurukuta mbele ya Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita jijini Dar, Nisha alifunguka kwamba mama yake ndiye kila kitu kwani muda mwingi humshauri mambo mazuri na ya kimaendeleo zaidi tofauti na mashosti wa mjini.
“Niacheni na mama yangu mzazi, kwa sasa ndiye shosti wangu mkubwa japokuwa nazungumza na kila mtu,” alisema Nisha ambaye alishawahi kuwa shosti mkubwa wa Flora Mvungi.