Friday, July 25, 2014

HIZI NDIZO UPDATES ZA TAARIFA YA NDEGE ALGERIA ILIYOPOTEA...!! ZISOME HAPA


Hizi ni updates nilizo nazo kuhusu ndege ya jana ya Algeria iliyopotea...Mabaki ya ndege hiyo iliyokuwa na watu 116 yamepatikana nchini Mali karibu na mpaka wa Burkina Faso

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na abiria 116 ikitokea Burkina Faso kwenda mjini Algiers, Algeria, yamepatikana nchini Mali, wamesema maafisa.
Jeshi la Burkina Faso limesema ndege hiyo ya shirika la ndege la taifa, Air Algerie, ilianguka karibu kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkinabe.
Waongoza ndege walipoteza mawasiliano na ndege hiyo mapema siku ya Alhamisi baada ya marubani kuripoti mvua na upepo mkali.
Miongoni mwa abiria hao ni raia 51 wa Ufaransa.

Ndege hiyo aina ya McDonnell Douglas MD-83- namba AH 5017, ilikuwa imekodishwa kutoka kampuni ya Uhispania, Swiftair.