Kichanga hicho kiliopolewa na wasamalia wema na baadaye kupelekwa katika kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Casa Della Diaia (Nyuma ya Furaha) na sasa kimetimiza mwezi mmoja tangu kikabidhiwe katika kituo hicho na hali yake ya kiafya inaendelea vizuri.
Wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Aloyce Gonzaga, Parokia ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji Luhanga Jimbo Kuu la Dar es Salaam walibahatika kutembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali wakiwa katika ziara ya kutembelea parokia tarajiwa ya Mtakatifu Yohana Mbatizaji ya Jimbo Katoliki la Chumbageni mkoani Tanga.
Kituo hicho kina jumla ya watoto 47, mtoto mkubwa akiwa na miaka 22 na mdogo ana mwezi mmoja.