Saturday, July 26, 2014

MABAKI YA NDEGE ALGERIA AH5017 YAONEKANA NCHINI MALI.

Mabaki ya Ndege ya Algeria baada ya kuanguka jangwani na Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 kupoteza maisha.

Ndege ya Algeria iliyopotea ni sawa na hii ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6


Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.
Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27 kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso , Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga.
CHANZO: BBC SWAHILI