Sunday, July 20, 2014

MASHABIKI BARCELONA WAMVAA SUAREZ MTAANI, ILIKUWA...

MSHAMBULIAJI Luis Suarez alizingirwa na mashabiki wakati akipita mitaa ya Barcelona na mkewe Sofia Balbi jana.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay aliyejiunga na klabu hiyo ya Katalunya kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 75, alikuwa mwenye tabasamu pamoja na familia yake wakati mashabiki wakimpokea kwa furaha.
Nyota huyo wa zamani wa Wekundu wa Anfield aliyepigwa picha akisaini jezi ya shabiki mmoja ya Lionel Messi - Suarez anatarajiwa kuwa pacha wa Muargentina huyo msimu hiyo Nou Camp.
Kivutio kipya: Luis Suarez akiwa amezingirwa na mashabiki mitaa ya Barcelona na mkewe Sofia Balbi
New signing: Suarez signs one Barcelona fan's Lionel Messi shirt on Saturday afternoon
Suarez akisaini jezi ya shabiki mmoja wa Barcelona ya Lionel Messi jana mchana

Wakati mashabiki kadhaa wa Barcelona walimzingira mchezaji wao huyo mpya, Suarez hawezi kupata fursa ya kutambulishwa rasmi baada ya kusajiliwa katokana na kufungiwa na FIFA kujihusisha na soka kwa meizi minne kufuatia kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini wakati wa mechi baina ya Uruguay katika Kombe la Dunia nchini Brazil