Friday, July 25, 2014

MICHEPUKO NOMA!! NJEMBA LAFUMANIWA GESTI ILIYOPO MBEZI AFRIKANA LIKIWA UCHI NA MKE WA MTU...ATANDIKWA KIPONDO CHA USO DAMU CHAPACHAPA


Mjomba wa Kelvin(Joseph) akimsihi Mpwa wake amsamehe mara baada ya kukutwa gesti na mke wa Kelvin.

TIMBWILI la aina yake lilifumuka ndani ya gesti moja iliyopo Mbezi Afrikana jijini Dar es Salaam (jina kapuni), kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina moja la Kelvin kumkuta chumbani mtu aliyedai ni mjomba wake, Joseph akiwa na mkewe wa ndoa, Emiliani.
Mkasa huo wa ajabu ulijiri usiku wa Jumamosi iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo Mbezi ya Afrikana jijini Dar es Salaam.
MPISHI WA FUTARI AUZA ISHU
Mama mmoja aliyedai ni mpishi wa futari maeneo hayo, alipiga simu kwa paparazi na kusema:
Kelvin (kulia)'akidili' kisawasawa na mjomba wake. 
“Mimi ni mpishi wa futari hapa Mbezi Afrikana kuna baba mmoja na ndugu zake wanachakazana, kisa wamefumaniana kwenye gesti ya (akaitaja jina). Ipo hapahapa jirani njooni muwahi.”
Mlinzi wa gesti akijaribu kumzuia Kelvin asizidi kumjeruhi mjomba wake.
 AIBU!
Paparazi walifika eneo la tukio ambapo walimkuta Kelvin amemvaa mjomba ‘ake chumbani ambapo timbwili zito lilitifuka. Walikuwa wakigaragazana huku mjomba mtu huyo akiwa kama alivyozaliwa na damu chapachapa jambo lililomtia aibu!
Mjomba akiwa chumba cha gesti mara baada ya mkong'oto 'hevi' kutoka kwa mpwa wake.
PICHA ZA TUKIO
Paparazi bila kuzubaa nae alianza kuchukua picha za tukio  hatua kwa hatua. Wakati Timbwili likiendelea, Joseph alikuwa akipiga mayowe kumuomba mpwa wake huyo amsamehe ili wayamalize kimyakimya na kumsihi asisambaze habari hizo zikafika mpaka nyumbani kwa mke wake.
MKE ATIMKA KINYEMELA
Katika hali ya kushangza, wakati wawili hao wakiendelea kuangushana chumbani, mke huyo alipata upenyo na kuchoropoka, akatimua mbio kwa kuhofia kipigo na kukwepa kamera za paparazi.
...Mjomba taratiiibu 'akirejesha' mavazi mwilini mwake.
MLINZI WA GESTI
Timbwili la wajomba hao lilitulizwa na mlinzi wa gesti hiyo (jina halikujulikana)  ambaye alitumia mabavu na kufanikiwa kuwadhibiti na kuwaweka kitako.
MJOMBA MTU AGOMA KWENDA POLISI
Baada ya kutulizwa, Kelvin aling’ang’ania waende polisi lakini mjomba mtu alikataa katakata akimbembeleza mpwa wake kwamba wayamalize na kuahidi kutorudia tena mchezo huo huku akisema mwanamke huyo alimuwekea mtego wa makusudi.
Mjomba akiomba msamaha kwa mpwa wake.
CHONDECHONDE KELVIN
Baadhi ya waungwana waliofika kushuhudia tukio hilo walimsihi Kelvin kumsikiliza mjomba ‘ake na kupokea fidia kidogo kwani kuyasongesha mbele mambo hayo ni aibu kwa familia yao na kumtia matatani mjomba huyo kwa mkewe.
MJOMBA ‘AJIKOMITI’ KIMAANDISHI
Kufuatia maombi ya watu, akiwemo mlinzi wa gesti hiyo, Kelvin alikubali kumsamehe mjomba wake ambaye naye ‘alijikomiti’ kimaandishi (kopi tunayo) kumlipa Kelvin fidia ya shilingi laki tano (500,000) na kuahidi kutorudia kummendea mke wake.
Sehemu ya nyaraka ikionyesha mjomba 'akijikomiti' kimaandishi.
Katika barua hiyo aliyoaindika Joseph kwa mkono, alikiri kukutwa na mke wa Kelvin na kusema anatoa shilingi laki tatu (300,000) siku hiyo kisha kiasi kinachobaki atatoa siku inayofuata.
MGONI AGEUKA NA KWENDA KUFUNGUA KESI
Hata hivyo, taarifa zilizotufikia zinadai kuwa, Joseph alikwenda kituo cha polisi (jina halijajulikana) kumfungulia kesi mpwa wake Kelvin na mkewe Emiliani akidai walipanga kumfanyia fumanizi.