Saturday, July 19, 2014

NYIE AKINA CHID BENZ, DUDUBAYA, TID: KAMA NGUMI PIGANENI NA MATUMLA, KASEBA AU CKEKA SIO KUWAPIGA WANAWAKE TU!!

Ukatili wa kijinsia haukubaliki hata kidogo, wengine tunapambana usiku na mchana kutokomeza vitendo hivi vya Ukatili na Udhalilishaji, cha ajabu watu maarufu sasaivi wamechachamaa kuendekeza vutendo hivyo.. 
 
Mara Dudubaya kampiga Mke wake, mara Tid kamtukana RayC, Mara Chidbenz kampiga mzazi mwenzake, mara Ezden kampiga mkewe, mara Chidbenz kampiga RayC!!!! jamani jaman jamani kwanini mnachukua uamuzi huo wa kudhalilisha Wanawake???
 
ChidBenz, Tid, Ezden na Dudubaya nyie ni vioo kwenye jamii yetu, kwahiyo si vyema kufanya vitendo vya kuwapiga Wanawake na kuwadhalilisha…kwani nyie hamkoseagi? kuna siku mmepigwa? sisi sote ni watu wazima kwa hiyo kama tumeshindwana kila mtu anachukua 50 zake kwa Amani…..
 
Kuna msemo unasema kwamba Mwanaume wa kweli hapigi Wanawake wala kumdhalilisha Mwanamke kwa sababu Wanawake ni Mama zenu. vitendo mlivyowafanyia hao Wanawake mngependa Mama Zenu wafanyiwe???
MAJERUHI
 

Ushauri

Kama wewe unajiskia kupigana basi ni vyema ukaomba pambano na Matumla, Kaseba au Cheka ili tujue kama kweli wewe ni mpigaji..kinyume na hapo ni kuonea Wanawake na kuwadhalilisha kijinsia….
 
Nawaheshimu sana kama wasanii lakini naomba mjirekebishe tena kuanzia sasa muwe mabalozi wa Kupambana na vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji kwa Wanawake. na muwaombe radhi wale mliowapiga na kuwadhalilisha..
 
Nipo  tayari  kushirikiana  na  nyie  kuhakikisha  kuwa  tunatokomeza  vitendo  vya  kikatili na  udhalilishaji  kwa  wanawake…..
 
Ney wa Mitego naomba useme na hawa mastaa wenzako ambao naona hawajasikia ule ujumbe wako kwamba Mwanamke hapigwi na mangumi na mateke…Waeleze Mwanamke anapigwa na nini…
 
Nakuita pia Linex utukumbushe ule ujumbe wako kwamba ndoa haivunjwi na mwanamke pekee bali hata Mwanaume nae aweza vunja ndoa.
 
Sasa inapotokea mmeshindwa kuelewana au kukubaliana haifai utumie Nguvu dhidi ya Mwanamke wako.. Kama mkishindwana mnaachana kwa Amani, msiachane na kutuachia Mangeu…