Mwili wa Mawazo Wilbard Kazungu (31) ukiwa nyumbani kwake ukining'inia baada ya kujinyonga katika chumba cha kulala watoto wake .
Eneo la chumba ambako alikaa kitandani na kunywa dawa ya kuoshea mifugo kisha kupanda stuli na kujitundika kamba |
Vijana walio kuwa na ukaribu na marehemu wakiwemo ndugu zake wakiubeba mwili wa marehemu kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi chini ya jeshi la polisi |
Alidai kuwa katika maisha ya kijana huyo alikuwa ni mjasiliamali wa kuuza mifugo na mazao mbalimbali katika kata ya mabawe kwa kujiongezea kipato kiuchumi na alikuwa hajashtakiwa kwa dhuluma bali aliishi vema na wananchi wake pamoja na jamaa wakiwemo marafiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mukaliza Manase Rutegama amesema kuwa marehemu mawazo wakati wa uhai wake hajawahikuwa na ugomvi wa kifamilia na alikuwa akifanya shughuli bila kuwa na migogoro yoyote.
"Viongozi na wanafamilia tumepokea kifo hicho kwa mshituko na katika kata ya mabawe wananchi walikuwa hawajapata kupata mtu aliyejinyonga na huyo kijana kaacha watoto watatu na mke mmoja".Alisema Rutegama.
Katika kutungua mwili wa marehemu kwenye kamba chini ya jeshi la polisi mganga mfawidhi wa kituo cha afya mabawe Juvent John alisema kamba ndiyo ilikatisha maisha yake baada ya kuziba mishipa ya damu na kukata mawasiliano ya kupumua
Hata hivyo jeshi la polisi licha ya kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho limewataka wananchi kuwa na ulinzi shirikishi kuhakikisha kila mmoja anatambua shda za mwenzake na kutoa taarifa katikavyombo vya dola kwa yule aliye na maoni ya kutaka kujiondoa nafsi yake ama kufanya matukio ambayo ni makosa ya jinai.
mmoja wa askari polisi jamii aliyetambulika kwa jina la Oscar alisema katika jeshi la plisi kuna dawati la ushauri nasaha kwani matukio ya kujinyonga wilayani Ngara yanazidi kuongezeka hasa kwa kuhusisha kundi la vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Alisema wanaobaki wakiteseka kutokana na matukio hayo ni akina mama na watoto na wazee waliokuwa wategemezi wa vijana hao na wananchi kwa imani zao hawana budi kusali pamoja kuomba Mungu kuepusha jinamizi hilo la watu kujinyonga.