CHUKUA tano! Staa sinema za Kibongo, Salma Salim ‘Sandra’ amesema kuwa kutoka moyoni mwake anamkubali msanii mwenzake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ baaada ya kupewa nafasi ya Ukatibu Kata ya Bwawani, Kinondoni jijini Dar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akipiga stori mbili tatu na mwandishi wa gazeti hili, Sandra alisema Steve Nyerere ni mtu ambaye anaweza kuwa kiongozi mahiri kwenye sekta mbalimbali ndiyo maana hata katika nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie ameleta maendeleo.
“Uongozi wa Steve ulianza kuonekana siku nyingi ndiyo maana wana-Bongo Movie tukamchagua na wakazi wa Bwawani nao wamempa ukamanda,” alisema