Mwenyekiti wa Club ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' ndoto yake ni kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwa Rais kwani uwezo wa kuwaongoza watanzania anao.
Akizungumza msanii huyo amesema kuwa kitendo cha kuchaguliwa kuwa katibu kata ya Bwawani, Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia chama cha Mapinduzi CCM, ni mwanzo mzuri wa kuelekea kutimiza malengo yake...
"Hakuna aliyezaliwa akitambua kuwa siku moja anaweza kuwa miongoni mwa viongozi wakubwa katika nchi hii, lakini dalili za kuwa huko huja kutokana na kuwa na malengo mazuri na kujitambua kama unaweza kuwaongoza watu wengine," alisema Steve Nyerere.
Msanii huyo alisema hakuna kiongozi anayeweza kushika nyadhifa za juu bila kuanzia chini kama alivyoanza yeye na ndio maana wabunge wengi huwa wanaanzia chini na taratibu wanakuwa wanapanda ngazi kwa lengo la kuona uwezo wao wa kuongoza