Thursday, July 3, 2014

TUZO ZA BET ZAZIDI ZILE ZA MTV KWA KUTAZAMWA NA WATU MILIONI 7.9...SOMA ZAIDI

nicki-minaj_1

Huenda ilikuwa ni sababu watu walitegemea kuwaona Beyonce na Jay Z ama tumbuizo lililosubiriwa kwa hamu kutoka Chris Brown baada ya kutoka jela, lakini vyovyote ilivyokuwa, tuzo za BET zilizofanyika Jumapili iliyopita ziliangaliwa na watu milioni 7.9.
Idadi hiyo ni kuwa zaidi tangu mwaka 2009 – mwaka ambao BET ilifanya maadhimisho ya Michael Jackson. Tuzo za BET ziliwazidi kwa mbali wapinzani wake, MTV Awards, ambao walipata watazamaji milioni 3.2.

Pia tuzo hizo ziliongelewa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kuliko hata Billboard Music Awards, Golden Globes, People’s Choice Awards, fainali za NBA ama mechi ya kombe la dunia kati ya Ureno na Marekani.