MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika, amewashangaza wapita njia baada ya kuonekana akitembea huku akipiga kelele katika mitaa ya Kariakoo.
Mwanamke huyo aliyekuwa amebeba boksi huku juu yake kukiwa na samaki wadogo wadogo, kitunguu, kipande cha chungwa na vinginevyo, aligeuka kituko baada ya kelele zake kuwashangaza wapita njia waliokuwa wakimuangalia na wengine wakimpisha njia kwa kumhofia. Hata hivyo, haikufahamika mara moja tatizo la mwanamke huyo.
-GPL