Amekiri kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’ ambayo wengi wanaitafsiri kwamba ni dini ya kumwabudu shetani kitu ambacho kiliwahi kukanushwa na aliyewahi kuwa mmoja wa viongozi wa freemasons Tanzania.
Mama anasema alimketisha Nay chini baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka ambapo baadhi ya picha sio za kawaida mfano damu pamoja na alama zilizotumika ndani yake.
Amesema ‘Naitwa Matilda Mwaipopo ni mama mzazi wa Nay, kwakweli mwanangu namchukulia lakini sifa tu zinazokuja kama Nay kwenye magazeti, Nay freemason, watu wanakuja wananisimamisha…. mwanao Nay kweli? mbona tunasikia freemason? basi kichwa changu kinapagawa…. ‘

‘Nikiangalia miziki anayoifanya kama hii aliyoitoa juzi, jamani mwanangu anaambiwa freemason usikute kweli freemason, Nay wa Mitego nimemuita…. mwanangu vipi? ninayoambiwa ni ya kweli? Freemason wewe? mbona wimbo wako huu siuelewielewi? ananiambia mama mimi sio freemason, namwambia hapana mwanangu hapana….. nasikia freemason watu wanatoaga hata wazazi sadaka’
‘Mimi ndio mama niliebakia baba yenu alifariki aliniacha ukiwa na miaka mitatu nimejitahidi kukulea mpaka leo…… unitoe sadaka mama yako kweli?????!!! Nay wa Mitego sana ni kucheka…… anaona tu mama kama anapagawa, lakini kwakweli mwanangu simuaminiamini miziki yake hii anayoifanya’