Monday, September 22, 2014

FLORA MVUNGI: MVUNGI NDOA MWAKA MMOJA, MTOTO MMOJA


Dada nakukubali sana, vipi kuhusu kiwango chako cha elimu? Fura, Hedaru, 0714403227
FLORA: Nina elimu ya kidato cha sita na Diploma ya Uandishi wa habari.

Msanii wa Bongo Muvi na muziki Bongo, Flora Mvungi akiwa na mwanaye Tanzanite.
NDOA NA UIGIZAJI
Hivi dada Flora unawezaje kuitumikia ndoa yako kikamilifu huku ukijishughulisha na uigizaji? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
FLORA: Ni kujipanga tu, yote yanawezekana.
MPANGO
Flora wewe ni msanii mahiri wa filamu Bongo, je, una mpango gani wa kujiendeleza kuhusiana na uigizaji? Salim Liundi, Dar, 0659601205
FLORA: Nafikiria bado sijajua.
MAISHA YA NDOA
Nakukubali sana Flora, je, kuna utofauti gani unaoupata katika maisha yako baada ya ndoa? Salma Hemedi, Dar, 0714189466
FLORA: Nimejitambua zaidi, mwanzo tulikuwa tunakula bata sana lakini kwa sasa tunakula huku tunamfikiria mtoto wetu Tanzanite.
UNDUGU 
Flora hivi wewe una undugu na yule Dokta (Sengodo) Mvungi aliyeuawa na majambazi? Muddy Madiley, 0652672805
FLORA: Ni baba yangu mdogo.
UKIMYA
Naipenda sana kazi yako ila una muda mrefu huja-ekti muvi au ndiyo kulea kwenyewe na mwanao anaitwa nani? Ester, Songea, 0769782090
FLORA: Mwanangu anaitwa Tanzanite, ni kweli kulea kumechangia kuwa kimya.


Flora Mvungi  akiwa na mume wake H-Baba.
KUVAA KIHASARA
Nakupenda sana Flora lakini sijui kwa nini unapenda kuvaa kihasarahasara? Everin, Moro, 0713390021
FLORA: Ilikuwa ni kabla ya ndoa siyo sasa.
ANAPENDA NINI?
Dada Flora ni kitu gani unachopenda kufanya tofauti na sanaa na vipi kuhusu mafanikio yako kwenye tasnia ya filamu? Rich, Dar, 0714868843
FLORA: Napenda sana kucheza na mwanangu, mafanikio ni ya kawaida tu.
MUZIKI
Flora ni kitu gani kilichokuvutia kuingia kwenye gemu la muziki? Fresa, Iringa, 0659868893
FLORA: Muziki naupenda sana muda mrefu na niliona nina kipaji hicho nikaona nikifanyie kazi.
KUHUSU MUMEWE KUOA?
Flora nasikia mume wako H-Baba (Hamis Ramadhan) aliwahi kumuoa Irene kwa mkataba wa miezi mitatu kisha wakaachana, ni kweli? Pili Abeid, Mbeya, 0756951612
FLORA: Siyo kweli.
ETI KWAO UGWENO?
Flora eti wewe ni mwenyeji wa Ugweno, Kilimanjaro? Msomaji, 0652303000
FLORA: Hapana, mimi kwetu ni Usangi (Kilimanjaro).
MAFANIKIO
Flora kiroho safi wewe ni msanii mzuri kunako gemu la sanaa, je, unazungumziaje mafanikio yako kuhusiana na sanaa tangu miaka iliyopita? Stellah Hegga, Dar, 0713737606
FLORA: Mafanikio ni ya kawaida tu bado naendelea kutafuta.
BONGO DAR ES SALAAM
Hivi kundi lenu la Bongo Dar es Salaam limefia wapi? Asha, Dar, 0652529062
FLORA: Kundi lilivunjika.
KUDUMU KWENYE NDOA
Flora umedumu kwenye ndoa kwa muda gani na mtoto wako anaitwa nani? Abdurahman, Moshi, 0756095555
FLORA: Ndoa ina mwaka mmoja sasa, mtoto anaitwa Tanzanite.
HUYU ANAMFAHAMU
Mimi nakufahamu, tulisoma shule moja, darasa moja katika Shule ya Msingi Mpakani Mabibo (Dar). Derick Waluya, Dar, 0652047905
FLORA: Ni kweli.
BIFU
Eti kuna taarifa zinazagaa kuwa wewe na Irene mna bifu, mliwahi kumgombea H-Baba. Msomaji, 0684980589
FLORA: Sina bifu naye na sijawahi kugombea naye H-Baba