Tuesday, September 30, 2014

HATUTAKI KATIBA MPYAA NG'OOO...MAUSTADH WAFUNGUKA


SHURA ya Maimamu Tanzania imetangaza hatua za kuikwamisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwa kwenda kuwaeleza waumini wa dini ya Kiislamu kupiga kura ya hapana.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge, kuiweka kando Mahakama ya Kadhi.

Akizungumza na MTANZANIA jana mara baada ya kumalizika kikao cha maimamu wa 

nchi nzima, Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, alisema hatua ya kupiga kura ya hapana ni moja ya azimio lililoafikiwa na kikao hicho.

“Msimamo wetu kwa asilimia 100 ni hapana, hatuungi mkono, tunalaani vikali jinsi mchakato huu wa Katiba ulivyovurundwa kwa sababu maoni ya Waislamu hayakuzingatiwa.

“Leo (jana) tulikuwa na kikao kilichojumuisha maimamu wote kutoka Tanzania na msimamo wetu katika hilo ni hapana,” alisema Sheikh Katimba.