Monday, September 29, 2014

KABURI LA MAREHEMU RECHO LALOA MACHOZI YA WAOMBOLEZAJI

Roho inauma ! Kwa mara nyingine , kaburi la
aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel
Leo Haule ‘ Recho ’ (pichani ) limeloa machozi
ya mastaa wakati wa kusimikwa msalaba
baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa ,
Ijumaa Wikienda lilikuwepo . Ibada hiyo iliyoambatana na kuombewa na
kutakaswa kwa msalaba huo, iliongozwa na
Mchungaji Mtweve na baadaye walielekea
Makaburi ya Kinondoni, Dar lilipo kaburi
alilopumzishwa Recho.
Walipofika makaburini , mastaa hao walijikuta
wakiangua vilio huku baadhi yao wakizimia
kwa kumkumbuka mpendwa wao. Kuna wakati Odama alishindwa kuvumilia
kulisogelea kaburi kwani aliangua kilio
kilichosababisha mama wa Bongo Muvi ,
Herieth Chumila kumzuia kwa kuhofia
kuishiwa nguvu. Mwisho, Odama na aliyekuwa
mchumba wa Recho , Saguda George walitoa
neno la shukrani kwa watu wote waliofika eneo
hilo na kuomba ushirikiano kwa lolote
litakalotokea .