Alisema saa 12 jioni siku ya jumapili ,alimtuma mtoto huyo kwenda dukani kuchukua simu, lakini binti yake alichelewa kurudi na aliporudi akamwambia mama yake kuhusu alichotendewa na Amoni Samwel.
Alichanganyikiwa baada ya kupata habari hiyo kutokana na hofu na hisia hasi kutoka kwa jamii na alipomchunguza aliona akitokwa na damu nyingi sehemu nyeti ambazo zilitapakaa kwenye makalio ndipo akampigia simu baba yake kabla ya kwenda kwenye vyombo vya sheria.
Alitoa taarifa katika kituo cha polisi cha wilayani hapo na kuandika mashtaka na kupewa PF3 kwa ajiri ya kupata matibabu katika kituo cha afya cha wilayani hapo na kufanyiwa vipimo vyote hasa ukimwi na magonjwa ya zinaa .
Wakati huohuo Chama cha wandishi wa habari (Tamwa) waliwasihi wandishi wa habari kanda magharibi wajikite kuibua habari zenye viashiria vya ukatili wa kijinsia hasa ubakwaji na ndoa za utotoni.
Kwa upande wa mwanafunzi husika (linahifadhiwa,) alisema kuwa baada ya kutumwa na mama yake alikutana na mwanafunzi mwenzake wa kiume na kumuomba amuelekeze walichofundishwa darasani na ndipo Amoni Samweli alipowakuta.
Aliwauliza walichokuwa wanafanya, nao wakamjibu kuwa wanasoma ghafla Amoni akaanza kumpiga makofi yule mwananfunzi mwenzake sanjari na kumfukuza eneo lile na kumshikia kisu na kumbeba juu juu na kumpelekea katika shamba la migomba na kumtendea unyama huo.
Nae Afisa Ustawi wa Jamii wa hapo Godfrey Kapaya alisema kuwa walifika nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kumfanyia vipimo vilivyothibitisha tukio hilo na alikuwa na majeraha sehemu za siri sanjari na kumpatia dawa za kupunguza maumivu, kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba” alisema Kapaya.
Kapaya aliongeza kuwa kwakuwa mwanafunzi alitakiwa kuingia kwenye mtihani walimpa ushauri wa kumuondolea hofu ili afanye mtihani akiwa katika hari nzuri ya kimawazo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Japhari Muhamed alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa tayari yuko mahabusu na hatua za kumfikisha mahakamani zinaendelea.ingawa awali kuna tetesi kuwa mtuhumiwa aliachiwa siku septemba ,8,2014ilihali alitenda kosa hilo siku ya 7,septemba 2014.
Na Magreth Magosso, Kigoma