Wednesday, October 29, 2014

AJALI YA KUTISHA JETI LUMO DAR

Gari aina ya Toyota Hiace inayobeba abiria ikiwa imekandamizwa na container baada ya kuangukiwa
Kumetokea ajali mbaya jioni hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami Wilaya ya Temeke jijini Dar ambapo gari kubwa la mizigo limeangukia Daladala iliyokuwa kituoni. Ajali hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
Mtoa taarifa wetu amesema hali ni mbaya na bado haijajulikana idadi ya vifo na majeruhi kwa ujumla. Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari zaidi.
Kuna gari la kunyanyua makontena limeshafika pale lakini limeshindwa kutoa msaada wa uhakika kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo likijaribu kunyanyua kontena kushuka chini na kuzidi kuongeza maafa.