millardayo.com iliahidi kuzifatilia hizi taarifa kwa Polisi ili kupata uthibitisho ambapo imefahamika ni kweli msanii huyu amekamatwa jana mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo baada ya alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Amesema ‘Alikuja Airport kwa ajili ya safari kwenda Mbeya, kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae na kijiko na yeye mwenyewe anakiri ni vitu vyake huwa anatumia ila anashangaa ni kwa nini vimeweza kubaki kwenye mfuko, tutamfikisha Mahakamani baada ya kuweza kubaini ni dawa aina gani za kulevya’