Thursday, November 6, 2014

BABA MTOTO WA ROSE NDAUKA MALICK: MWACHENI ROSE NDAUKA AJIRUSHE

BAADA ya msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka kuonekana akijiachia viwanja mbalimbali tofauti na alivyokuwa akiishi awali, mzazi mwenzake, Malick Bandawe, ameibuka na kumfungukia kuwa aachwe ajirushe.
Malick Bandawe.
Malick alifungua kinywa kufuatia madai kwamba alipokuwa akiishi na Rose alikuwa akimpa sheria kali na kumkataza kwenda ‘out’ ndiyo maana alikuwa hajiachii kama ilivyo sasa na hiyo ni moja ya sababu zilizosababisha uhusiano wao kuvunjika.
“Mimi siyo mkali wala sina sheria hizo ninazoambiwa ila nilikuwa nachukua muda mwingi sana kuzungumza na Rose na ninaamini amejifunza mengi sana mazuri ambayo akiyazingatia yatamsaidia maishani.

Msanii wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
“Sababu za Rose kujiachia hivyo ni kutokana na maisha ambayo tulikuwa tunaishi hivyo anahitaji muda atatulia na atakuwa sawa na hapo ndipo atakapoanza kuyafanyia kazi yale mazuri aliyoyapata kutoka kwangu, sitegemei yeye kufanya mabaya ila nategemea afanye mazuri kwa ajili ya mtoto wetu,”alisema Malick.