Tuesday, November 18, 2014

MADAKTARI WACHANA CHANA KWA WEMBE UUME WA MWIZI WA SIMU KISHA KUMCHAPA VIBOKO HADI KUFA

Polisi nchini India wanasema kuwa kikundi cha madaktari kimempiga hadi kufa mshukiwa wa wizi katika taasisi ya mafunzo ya udaktari mjini Calcutta mashariki mwa India.
Mwanamume huyo alifungwa kwenye mlingoti na kucharazwa viboko huku uume wake ukikatwakatwa kwa wembe.

Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo alidaiwa kuiba simu za mkononi. 
Watu wawili wamezuiliwa na polisi huku uchunguzi ukiendelea kufanywa.
Wandishi wa habari wanasema kuwa mauaji hayo ni dalili ya tatizo la watu kuwaadhibu washukiwa wa uhalifu nchini India hadharani.
Lakini kinachoshangaza sana katika tukio hili ni kuhusika kwa madaktari katika kitendo hicho.
Madaktari hao walimburuza mwanamume huyo hadi katika chumba kimoja cha hospitali hiyo na kuanza kumshambulia kabla ya kumuacha akiwa hali mahututi ambapo baadaye alifariki.


Baadhi ya madaktari walimshambulia mwanamume huyo katika sehemu zake za siri na kumkatakata kwa wembe kitendo ambacho kimewashtua wengi.