Majambazi watatu ambao bado hawajafahamika walivamia nyumba anakoishi kiungo mshambuliaji wa BafanaBafana Sibusiso Vilakazi ambako walipora vitu kadhaa vya thamani.
Kwa mujibu wa ripoti iliyothibitishwa na mchezaji mwenyewe, majambazi hao walivamia nyumba ambamo mchezaji huyo anaishi na wanae na walimuulizia mchezaji huyo kiasi kwamba ikaonekana kabisa walipanga kumdhuru.
Vilakazi ambaye ni nahodha wa klabu ya Bidvest Wits ameelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo hasa ukizingatia kuwa bado hajasahau kilichomkuta mchezaji ambaye alikuwa akilala naye kwenye chumba kimoja kwenye kambi ya timu ya taifa Senzo Meyiwa.