Thursday, November 27, 2014

MAMA MJANE ANA SIKU TATU HAJATOKA NJE AKIDAI KUTISHIWA KUUWAWA KISA ARDHI

MAMA mmoja makazi wa Kwembe, jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la mama Aureria Emmanuel Msuya ambaye pia ni mjane amejikuta akishindwa kutoka nje ya  nyumba yake na kubaki akijifungia ndani kwa muda wa siku tatu baada ya kudai kutishiwa na baadhi ya wananchi pamoja na wanajeshi ambao wanafanya kazi ya kusawazisha katika kiwanja kinachopakana na eneo lake.
Akizungumza na waadishi wa habari alisema ‘Mimi niko hapa toka mwaka 1988 baada ya kustaafu nilinunua hiki kiwanja, leo hii nashangaa  nguzo nilizoweka kama mipaka imeng’olewa bila taarifa na ninaona wanazidi kusogea katika eneo langu, mbaya zaidi nimeaambiwa nisitoke nje nitavurugwa au kuuliwa kwa dakika chache’’ alisema  mama Msuya.
Aidha mgogoro huo wa aridhi umefikishwa mahakamani na kutolewa hati ya kutaka kusimamishwa shughuli zote katika uwanja huo lakini wahusika wameonekana kukaidi na kuendelea kufanya shughuki kama kawaida, huku kiwanja hicho kikishindwa kutolewa maelezo sahihi na viongozi wa eneo hilo, wengine wakidai ni eneo la Serikali, CCM na wengine wakidai ni kiwanja cha vijana wa eneo hilo la Kwembe.
Mama Aureria Msuya (mjane) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waandishi wa habari wakizungumza na mama huyo(hayupo pichani) akiwa kajifungia ndani.
Mtendaji wa kata ya Kwembe Idd Mnyeke.
Muonekano wa nyumba ya mjane huyo inavyoonekana.