Tuesday, November 18, 2014

MAPICHA:MAMA AWAKIMBIA WANAYE WENYE KIFAFA



Bw. Nabo Philipo aliyekimbiwa na mkewe.
HILI nalo ni tukio! Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Nabo Philipo ameibuka na kudai kuwa, mkewe Mariana Thomas Silayo (pichani) amekimbia nyumbani na kumwachia watoto wawili wenye ugonjwa wa kifafa.
Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili hivi karibuni, Nabo alisema alifunga ndoa na Mariana mwaka 2002 na kujaliwa kupata watoto wawili, Madelin  na Joyce Nabo na ndani ya miaka 13 ya ndoa waliishi kwa amani.
Mke wa  Bw. Nabo Philipo, Mariana Thomas Silayo.
“Visa vilianza hivi karibuni baada ya mimi kupata hundi ya shilingi milioni 50 kupitia kazi zangu za ufundi wa kusuka mashine za magari, za kusaga na kukoboa na za matofari.“Nilimuonesha mke wangu hundi ili tupange tuzifanyie nini fedha hizo, lakini baada ya siku mbili hundi ikiwa benki kusubiri iwe tayari kutumika, nilianza kuumwa vitu visivyoeleweka na kuishiwa nguvu.
Mmoja wa watoto wa Bw. Nabo Philipo  na mkewe, Mariana Thomas Silayo.
“Nilikimbizwa Hospitali ya Aga Khan (Dar) na kugundulika kuwa nilipewa sumu kwenye chakula.
“Nilimuuliza mke wangu ni nani atakuwa ameniwekea sumu akasema sijui. Siku nyingine nilimkuta ana dawa za ajabuajabu, nikamkalisha chini na kumsema aachane na habari za dawadawa.
“Nilishangaa sana kwani mambo mengi mke wangu alianza kuyafanya kuanzia hapo. Niligundua pia kwamba  alikuwa akichukua nguo zake kidogokidogo na kuhamishia sehemu nyingine, ndipo siku moja akatoroka nyumbani moja kwa moja.
Mmoja wa watoto wa Bw. Nabo Philipo  na mkewe, Mariana Thomas Silayo.
“Kinachoniuma ni kitendo cha  kuniachia watoto wagonjwa, hasa huyu mdogo (Joyce) ambaye hushikwa na kifafa mara kwa mara, wakati mwingine humwangusha asubuhi na kumwachia jioni.
“Nilijaribu kumsihi mke wangu arudi kwa ajili ya watoto lakini kwake imekuwa ngumu. Nimeeleza haya ili jamii imfahamu ni mwanamke wa aina gani kwani  hana huruma, maana nilishangaa hata alipoondoka watoto walifurahi,”  alisema Nabo.
Mariana alipotafutwa ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo ya mumewe hakupatikana, waandishi wetu wanaendelea kumsaka.