Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping,wakati alipozuru bara Afrika.
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.
Rais Xi JinPing wa Uchina alizuru nchini tanzania mwaka uliopita
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu.Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.