Saturday, December 13, 2014

AUNT EZEKIEL: BORA NIZAE TU, UMRI UMEENDA!

NENO! Siku chache baada ya kuripotiwa kuwa ni mjamzito, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameibuka na kufunguka kuwa, aachwe azae kwani umri unazidi kuyoyoma.
Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Aunt alisema watu wamekuwa wakizungumza sana kuhusu ujauzito wake lakini kikubwa ni kwamba ameupata akiwa na umri sahihi na wala siyo chini ya miaka 18.
“Najua watu wengi wanazungumza kuhusu mimi na ujauzito wangu lakini mimi sijaona tatizo na tena siko chini ya umri wa miaka 18 sijui kama kuna tatizo lolote nikipata mtoto na hivyo kama mimba ipo watu wasubiri,” alisema Aunt ambaye amekuwa mzito kuanika umri wake hadharani.
Aunt ambaye aliolewa mwaka 2012 na Sunday Demonte anayedaiwa kusota nyuma ya nondo huko Dubai kwa msala wa madawa ya kulevya, kwa sasa anadaiwa kubanjuka kimapenzi na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo.
Hata hivyo, mimba hiyo ya Aunt haijajulikana kama ni ya Iyobo au mwanaume mwingine maana wawili hao wamekuwa wakichenga kuizungumzia.