Muongozaji, msanii na mmiliki wa Kampuni ya Filamu ya Five Effects, William Mtitu amewavaa wasanii wenzake wakiwemo Salma Jabu ‘Nisha’, Jacob Steven ‘JB’ na wengineo akidai wanatumiwa kuiua tasnia ya filamu Bongo kwa kukubali CD zao kuuzwa buku.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Mtitu alisema Kampuni ya Steps imeamua kuleta mitambo ya kutengeneza ‘CD’ za muvi na kuziuza kwa shilingi 1,000 sawa na muvi feki zinazouzwa mitaani ambapo alisema si vyema wasanii kukubali suala hilo kwani litasababisha tasnia nzima kushuka thamani.
“Madhara ya kuuza filamu zetu kwa shilingi 1,000 ni makubwa kwa baadaye, mimi nawashangaa hawa wasanii wenzangu kuunga mkono hilo. Hivi kwa namna gharama na uandaaji zilivyo juu, kuuza filamu kwa buku italipa kweli?” alihoji Mtitu na kuongeza:
“Kushushwa kwa bei ya filamu hakutaathiri wadukuzi peke yao bali hata sisi wasambazaji wazalendo kwa hiyo ni nyema tukaliangalia hili kwa macho matatu.”