Tuesday, December 30, 2014

NDOA YA ISABELA KARAMA YABUMA



Isabela Mpanda amesema kuwa anasikitika kuona mwaka umeisha mipango yake ya kufunga pingu za maisha na mwandani wake wa siku nyingi Luten Karama imegonga mwamba na kutamani kuolewa ndoa ya kimyakimya.
Msnii wa muziki Bongo, Isabela Mpanda akiwa na mpenzi wake Luteni Kalama.
Akizungumza kwa masikitiko mwanadada huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Ruvuma alisema, maisha ya uchumba yameshamchosha na ndiyo maana anapigania kuolewa, ambapo harusi yao ilitarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu, lakini kutokana na sababu zilizoshindwa kuzuilika ndoa imeshindikana hadi mwakani.
“Roho inaniuma sana natamani mno kuingia kwenye ndoa lakini kwa mwaka huu imebuma bila kutarajia, tulifanikiwa kufanya kikao kimoja tu cha harusi sasa nikafiwa na dada yangu ikabidi mipango yote isimame basi ndiyo kimya hadi sasa, nilimwambia Karama tuoane kimyakimya ndoa ya Bomani kisha sherehe itafuata akagoma, kwa hiyo tunatarajia kufunga pingu za maisha mapema mwakani Mungu akipenda,”alisema Isabela.