Thursday, January 29, 2015

ANGALIA PICHA- BIBI ANAYEDHANIWA KUWA MCHAWI AKUTWA AKIWA UCHI HUKO MAGEUZI MJINI SHINYANGA

 Bibi(aliyeko pichani) ndiyo amezua kizaa zaa baada ya kukutwa nje ya nyumba ya mkazi wa mtaa huo Suzana Mwandu akiwa uchi wa mnyama hajitambui huku akitembea kwa kutumia makalio yake-picha na Kadama Malunde-Shinyanga


Malunde1 blog iliyofika eneo la tukio haraka iwezekanavyo kama kawaida yake imeambiwa kuwa bibi huyo ambaye hakujulikana jina wala makazi yake awali alikuwa haongei na aliposemeshwa ndipo akaanza kuongea kwa lugha ya Kisukuma maneno yasiyoeleweka huku akisikika akisema wenzake wamemuacha alikuwa anaenda kwenye sherehe-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Hatimaye bibi akaweza kusimama na kuanza kufanya vituko vya kila aina
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akaamua kukaa na kuanza kutoa pesa alizokuwa amezifunga kiunoni kwa kwenye mfuko mlaini-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Zilikuwa ni shilingi za hamsini hamsini,mia moja ,mia mbili,mia tano na elfu akaziweka kwenye kibakuli kilichokuwa eneo la tukio
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Kushoto ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mageuzi Waziri Musa(CHADEMA) akisaidiana na wananchi wa eneo hilo kumwondoa bibi huyo kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akawekwa chini ya mti,hata hivyo akaendelea kufanya vituko na kuamua kulala juu ya mawe,angalia hapa chini-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Bibi akiwa amelala juu ya mawe kabla askari polisi hawajafika eneo la tukio leo mchana japokuwa bibi huyo amekutwa nyumbani kwa mtu saa moja asubuhi-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi wakimwangalia bibi huyo
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi wakitoa maelekezo kwa wananchi wa mtaa huo ambapo walisema serikali haiamini ushirikina hivyo kuwataka wananchi waondoke eneo la tukio na kumwacha bibi aendelee na safari yake kwani tayari alikuwa ameanza kutembea
-picha na Kadama Malunde-Shinyanga

Askari polisi akiwa amembeba bibi huyo kumtoa kwenye mawe,na katika hali ya kushangaza bibi huyo alimng'ang'ania askari huyo-picha na Kadama Malunde-Shinyanga